101 onlineHizi Ndio Laptop Bora za Kununua Mwaka 2016
Kama unatafuta laptop ya kununua ni vyema ukajifunza kwanza namna ya kujua laptop gani ya kununua kisha ukisha jua vitu vya kuzingatia itakua ni rahisi kuchagua laptop ambayo ingekufaa kati ya laptop hizi kumi bora ambazo zitafaa sana kwa matumizi mbalimbali kwa mwaka 2016.Laptop hizi zitakufaa kwa matumizi ya kila siku pia tumejitahidi kuweka na bei zake pamoja na mahali zinapo uzwa ili kurahisisha kama ungependa kununua.
Dell XPS 13
Dell XPS 13 ni laptop ya kisasa ambayo pengine ni laptop nyembamba kuliko laptop nyingine kwenye hii list laptop hii ina kioo kizuri chenye inch 13 pamoja na fremu ya inch 12 pia laptop hii ina uwezo wa hali ya juu sana kwani ina processor ya 6th Generation Core processor pamoja na hard disk ya SSD. Kwa upande wa chaji laptop hii inakaa na chaji kwa hadi masaa 12 ikiwa ilichajiwa ikajaa kabisa kingine kikubwa ni kwamba laptop hii ni nyepesi sana pengine ni kuliko bei yake.
Lenovo Ideapad 100S
Kwa wale tunao penda vitu vizuri vya bei nafuu laptop hii ya Lenovo Ideapad 100S ndio laptop ya kununua kwani pamoja na kwamba inauzwa bei rahisi sana lakini sifa za laptop hii hazifanani na bei yake kabsa, laptop hii ina inch 16 ikiwa inakuja na Window 10 pamoja na kioo bora angavu ambacho kinaifanya laptop hii kuwa bora kabisa. Laptop hii inauwezo wa kukaa na chaji masaa 9 ikiwa imechajiwa ikajaa pia inakuja na ofa ya Window Office 365 Personal.
Asus F555LA
Asus F555LA ni laptop ambayo inakuja na kioo angavu chenye uwezo wa 1080p pamoja na sauti nzuri ambayo hufanya laptop hii kuwa bora kabisa pia laptop hii ina 4GB za RAM pamoja na Processor ya Intel Core i3 ikiwa ni bora kwa kufanya kazi zako za kila siku.
Lenovo X260
Ikiwa ni laptop inayokaa na chaji pengine kuliko laptop hizi zote Lenovo X260 ina uwezo wa kukaa na chaji kwa karibia masaa 17 ikiwa imechajiwa ikajaa pia laptop hii ya 12.5-inch ni laptop bora kwaajili ya wafanya biashara pia ni ndogo na inauwezo wa kuingia na kutoshea kwenye mabegi ya aina mbalimbali.
Apple MacBook Air (13 inch
Pamoja na kwamba laptop mpya ya 12-inch Apple MacBook imetengenezwa kwa dizain nzuri lakini bado Apple MacBook Air (13 inch) ni laptop bora kabisa, ikiwa imetengenezwa na kava la aluminium yenye uzito wa pound 3 laptop hii ya Apple ni laptop yenye uwezo mkubwa kama watu wengi wanavyojua. Pia Laptop hii inauwezo wa kukaa na chaji zaidi ya masaa 14 ikiwa na uwezo mkubwa pamoja na kioo chenye uwezo mkubwa.
Lenovo ThinkPad T460
Ikiwa ina uwezo wa kukaa na chaji kwa masaa 13 ikiwa imechajiwa ikajaa laptop hii ya Lenovo ThinkPad T460 ni moja kati ya laptop ngumu za mwaka huu ikiwa na kioo cha inch 14 laptop hii imepita kwenye majaribio mbalimbali ikiwa kama yale ya Vibration test, Shock test pamoja na Extreme temperatures kwa hiyo kwa wale wanaotafuta laptop ngumu za kazi hii ndio laptop ya kununa.
Lenovo Yoga 900
Kwanini unununue laptop ya kawaida wakati unauwezo wa kununua laptop ya 2 in 1 Lenovo Yoga 900 inatumia processor ya 6th-gen Intel Core i7 CPU pamoja na kioo cha 13.3-inch 3200 x 1800 ikiwa imetengenezwa kwa dizaini ya kisasa kabisa, laptop hii inauwezo wa kubadilika kutoka kwenye laptop na kuwa Tablet ikiwa ni moja kati ya laptop yenye muundo unaokubalika sana duniani.
Asus ZenBook Pro UX501VW
Kama ilivyo Macbook laptop hii yenye uwezo wa kioo chenye 3840 x 2160 UHD Touch screen ni laptop bora kwaajili ya watu wanao tengeneza michoro mbalimbali kwenye kompyuta maarufu kama Graphics Designers, laptop hii yenye Processor ya Intel Core i7 CPU pamoja na kadi ya graphics ya Nvidia GTX 960M GPU ni moja kati ya laptop chache zenye uwezo wa ku-edit hata video ya 4K.
Alienware 17 R3 (2016)
Kama wewe ni mpenzi wa Michezo ya Kompyuta laptop hii ni chaguo zuri kwaajili yako ikiwa imeboresho zaidi laptop hii inatumia teknolojia ya Sci-fi ikwa pamoja na keyboard bora yenye rangi inayo endeshwa na Processor ya 6th Generation Core i7 CPU ikiwa pamoja na kioo chenye teknolojia ya 4K ambacho kinatumia graphics kadi ya Nvidia GeForce GTX 980M mobile GPU. Hii ni moja kati ya laptop bora za michezo ya kompyuta au game mpaka sasa.
Toshiba Chromebook 2 CB35
Kama unatafuta laptop nyepesi ya bei nafuu Toshiba Chromebook 2 CB35 ni laptop bora kwaajili yako ikiwa na kioo cha 13.3-inch pamoja na teknolojia ya HD display laptop hii ni bora kwa matumizi yako ya kila siku pia laptop hii ina kaa na chaji kwa zaidi ya masaa 10 pale itakapo chajiwa ika jaa kabisa.
Asus ZenBook UX303UA
Kama unatafuta laptop ndogo lakini yenye ubora Asus ZenBook UX303UA ni laptop bora sana kwaajili yako ikiwa inatumia teknolojia ya 1080p touch screen pamoja na processor ya Intel Core i5 CPU laptop hii ni kati ya laptop bora zenye umbo dogo pia laptop hii ina hard disk ya 256GB ikiwa inatumia teknolojia mpya ya SSD, kwa upande wa chaji Asus ZenBook UX303UA inakaa na chaji zaidi ya masaa 8 ikichajiwa ikajaa.
No comments:
Post a Comment