• Seynation Updates

    Saturday, 16 July 2016

    WIMBO WA NEY WA MITEGO 'PALE KATI PATAMU' WAFUNGIWA NA BASATA...NEY WA MITEGO APEWA ONYO KALI

    Tokeo la picha la pale kati ney wa mitego    Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) LIMEUFUNGIA rasmi mwimbo wa msanii NEY WA MITEGO- PALE KATI PATAMU, kutokana na ukiukwaji wa Maadili, na udhalilishaji wa kijinsia.
    Kutokana na Taarifa iliyotolewa na katibu mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, amesema kuwa msanii huyo amekua na tabia ya kuchafua sekta ya sanaa kwa manufaa yake binafsi.

    Mtendaji huyo amesema "Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambaba na kutoa lugha za matusi na kudhalilisha watu wa kada mbalimabali.."

    Pia ameeleza kuwa  mujibu wa kifungu 4(L) cha sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, baraza limepewa jukumu la kuhakikisha kuwa linalinda maadili miongoni mwa wasanii............."

    "Ikumbukwe kuwa BASATA imeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na kutoa kazi zisizo na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hio. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya ni uthibitisho kuwa hajabadilika na kwa maana hio ameendelea kuidhalillisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua nakuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi zingine......................."

    NINI MAONI YAKO??



    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI