Chama cha madaktari nchini Kenya kimetangaza kuwa hospitali zote zikiwemo za kibinafsi zitagoma kwa saa 24 siku ya Jumanne tarahe 13 mwezi huu, ikiwa serikali itashindwa kutekeleza makubaliano ya kuimarisha mishahara ta wafanyakazi wa sekta ya afya na mazingira yao ya kufanya kazi.
Mgomo huo uanoadhiri hospitali zote za umma kwa sasa uko siku yake na nne, baada ya serikali kushindwa kutekeleleza mkatana wa mwaka 2013 wa kuwapa madaktari nyongeza ya mshara ya asilimia 300.
Afisa mmoja wa chama cha madaktari Ouma Oluga, amesema kuwa madaktari kutoka hospitali kuu ya Kenyatta wamejiunga kwenye mgomo huo na kusitisha huduma zao tangu Jumatatu.
Chama cha madaktari kinasema kuwa kimejiondoa kutoka kwa mazungumzo yoyote na serikali na watarudi tu mezani kujadili njia ya kutekelezwa kwa makubaliano yao.
Makubaliano hayo yaliyoafikiwa mwaka 2013 yaliitaka serikali kuajiri madaktari zaidi na kuboresha vituo vya afya, makubaliano ambayo madaktari wanasema kuwa hajajatekelezwa.
No comments:
Post a Comment