Notisi hiyo ya masaa 24 ilizitaka kampuni zilizoko kwenye jengo hilo katika Kitalu Namba. 189/2 kwenye Barabara ya Nyerere kuwa ni Quality Group Company Limited, Gaming Management Limited, Q Consult Limited, Quality Logistics Company Limited na International Transit Investment Limited, ambazo ziko chini ya Manji kuondoka mara moja.
Hata hivyo sakata la Manji kutimuliwa lilianza kitambo akidaiwa kufanya biashara zenye utata na mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kufanikiwa kuiuzia PSPF jengo la Quality Plaza na Mufuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) maghala kwa shilingi bilioni 46, ambayo aliyajenga kwa mkopo wa Sh bilioni 9 kutoka mfuko huo.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa ijumaa ya Mwezi wa 4 ,2011 PSPF ilifanya maamuzi kama hayo baada ya kubanwa na Wabunge wa Kamati Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) enzi hizo sasa (PAC),iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ,ambae kwa sasa ni Mbunge wa Kigoma mjini (ACT).
SOURCE: Makorokocho.co.tz
No comments:
Post a Comment