• Seynation Updates

    Thursday 29 June 2017

    Kukamatwa Kwa Viongozi wa TFF na Takururu..Haji Manara Awatumia Pole ikiwa na Dongo Ndani yake



    Baada ya taarifa za kukamatwa kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Celestine leo mapema msemaji mkuu wa klabu ya Simba (aliyesimamishwa), Haji Manara ametoa pole kwa viongozi hao.


    Haji Manara amesema sisi kama wanadamu tunapitia changamoto nyingi sana hivyo ni bora tukafarajiana japo hata kwa kupeana pole pale mwenzio anavyopatwa na matatizo.

    Poleni Viongozi wangu wa TFF,no matter wat!!ni challenges tu ktk life, bnadaam hatufai kuombeana mabaya,hata kama huwakukutendea haki, Mungu awasimamie kutendewa HAKI,“ameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

    Haji Manara ambaye alipigwa ‘STOP’ na TFF ya kutokujihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja kwa makosa ya kinidhamu bado anaendelea na msimamo wake wa kuitumikia klabu yake ya Simba kama kawaida kwani alilitaka Shirikisho hilo limpe barua ya kumsimamisha.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI