• Seynation Updates

    Wednesday, 28 June 2017

    TID, QUICK ROCKA NA OMG WAMALIZANA KIBABE WASULUHISHWA NA AKINA B-DOZEN



    Siku chache zilizopita Quick Rocka na kundi la OMG waliachia video ya wimbo Watasema huku staa mwingine wa Bongofleva TID akidai wametumia melody na maneno ya wimbo wake bila ridhaa yake hivyo kutaka alipwe fidia ya Tsh. 20m.

    Sasa leo June 27, 2017 wasanii hao wamekutana ana kwa ana kwenye XXL ya Clouds FM ikiwa ni Eid Pili ambapo kila mmoja aliezea kilichotokea huku TID akiulizwa kama ni yeye ndiye aliyepost na kwa nini alichukua uamuzi wa kudai fidia na majibu yake yalikuwa hivi:

    ”Ukweli ni kwamba hawa jamaa walitakiwa wanilipe lakini tumekubaliana. Wamekuja tumepozana ili mwisho wa siku kuendeleza muziki mzuri. Nilipanic nikasema Rocka ndio anatoboa sasa hivi nitamuona na Lamborghini.

    “Halafu huu wimbo umechukua tuzo mbili, kama East Africa Best Collaboration Song na Best Video kwa kipindi kile. Ulikuwa wimbo mkali sana halafu ulinicost hela nyingi. Nilirecord Kenya, Home Boys walinicharge kama 1.5m za kitanzania kufanya kila kitu lakini mwisho wa siku nimeona kafanya kitu kizuri.

    Pesa siyo kitu sana kama ameweza kufanya A, B, C, D kwa lengo la muziki mzuri nimempa blessing zangu acha anunue Lamborghini.” – TID.

    Quick Rocka naye amesema TID ni mtu wa busara sana kwani walikaa chini na busara zikatumika ili mambo yakae sawa:“Tulikuwa na Vibe Studio baada ya kufanya nikamchek TID japo nilimwambia juu juu sikufunguka sana na ndio maana ilivyotokea ikawa hivyo lakini tukakaa chini mzee ana busara nyingi sana na zikatumika. Tumesalve issue imekuwa poa.” – Quick Rocka.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI