Pichani ni Tuzo ya Bi.Auleria Gabriel.
Bi.Auleria Gabriel ameshinda katika kipengele
cha uandishi wa habari za kodi na mapato nchini katika upande wa Radio akiwa ni
mshindi pekee kwenye nafasi hiyo aliye jinyakulia Ngao, cheti na hundi ya pesa.
Akizungumza na Mnanagyblog Bi.Auleria amesema
siri ya ushindi katika tuzo hiyo ni kujituma katika kazi kwa kuweka malengo na kufanya
kazi kwa ubora.
|
Pichani ni msdhindi wa tuzop hiyo Auleria Gabriel akiwa na tuzo yake.
“Kikubwa huwa ni kujituma kwa kutambua nini
unafanya wewe kama mwanahabari ili kuandika habari zinazoigusa jamii ya
watanzania kwani tupo kwa ajili ya kuisaidia jamii ambayo inatutegemea kwa
kiasi kikubwa kupata habari mbalimbali” amesema Bi.Auleria
|
Hata hivyo amewataka waandishi wa habari
nchini na wafanyakazi wenzake wa Radio kwizera kujikita katika uandishi wa
Habari unao lenga kusaidia jamii inayowazunguka ili kuleta mabadiliko chanya .
|
Tuzo hii kwa Bi.Auleria Gabriel ni ya pili tangu
aanze kazi yake katika kituo hicho cha matangazo Radio kwizera kwani
itakumbukwa kwamba mwaka 2016 alipata
tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia zilizo tolewa nchini Namibia, tuzo ambazo
zilishirikisha mataifa yaliyo kusini mwa bara Afrika{SADC} ambapo pia aliibuka mshindi
kwa upande wa Radio.
|
Habari picha ikimuonesha Bi.Auleria Gabriel baada ya kutwaa tuzo 2016 huko nchini Namibia |
Pichani Bi.Auleria Gabriel akitoa neno shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo yake huko nchini Namibia. |
Pichani
Bi.Auleria Gabriel akiwa na muwakirishi wake aliye ambatana naye kutoka
tanzania Bi.Gladness Munuo ambaye ni muwezeshaji kutoka taasisi inayo
shughurikia masuala ya Jinsia hapa nchini {GEMSAT}. Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA |
No comments:
Post a Comment