• Seynation Updates

    Saturday, 19 May 2018

    Viongozi Wa TFF Kukiona cha Moto- Paul Makonda

    Tokeo la picha la paul makonda

    Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema atachukua hatua kwa viongozi wa michezo ambao hawajafanya marekebisho ya uwanja wa Taifa wa ndani 'indoor' licha ya kuwakabidhi pesa na vifaa mwaka jana.

    Makonda amesema Mei 18, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa alikubali kujinyima na familia yake ikae gizani kwa kutoa jenereta la nyumbani kwake ili kutimiza ahadi ambayo aliwahidi wanamichezo hao lakini imekuwa kinyume na mategemeo.
    Lile jenereta nililihamisha badala ya kuwepo nyumbani kwa mkuu wa mkoa nikalikabidhi mwaka jana, sasa kama mpaka leo hii halijaenda basi kutakuwa kuna shida mahala, na niwaambie tu siwezi kuahidi kitu nisifanye hata kama ni cha kwangu nitajinyima, nimeinyima familia yangu wakae gizani ili nihakikishe kwamba jenereta linakwenda kwa wapenzi wa mpira” amesema Makonda.
    Makonda ameongeza kuwa atawasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ili aweze kuwachukulia hatua watu ambao wameshibdwa kutimiza majukumu yao
    Mkuu wa Mkoa Makonda amesema mwaka jana alikabidhi pesa, mipira, mabati na jenereta ili kusaidia uwanja wa Taifa wa ndani uliokuwa katika hali mbaya na hivyo anashangaa kusikia bado hakuna kilichofanyika mpaka sasa.

    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI