Zahanati Nne katika Tarafa ya Rulenge na Murusagamba Wilayani Ngara Mkoani Kagera zimepokea msaada wa dawa zenye thamani ya Shilingi milioni 15.4 kutoka kwa Kampuni ya kabanga Nickel wilayani humo.
Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo Bw.Francis Wikedzi amesema dawa hizo zitatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika zahanati za Mumiramila, Bugarama, Muganza na Mukubu ili wananchi wapate huduma nzuri za matibabu.
Bw Wikedzi amesema kampuni hiyo inahitaji kusaidiana na serikali ya wilaya na vijiji kusaidia kupunguza changamoto zilizopo katika kijamii.
Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara Bw Vedastus Tibaijuka ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wake na kwamba kampuni inashiriki kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu na Afya ili kuharakisha maendeleo ya wilaya.
Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment