• Seynation Updates

    Sunday, 27 December 2015

    ALSHABAB WAUA POLISI 2 NCHINI KENYA



    Maafisa wawili wa polisi wameuawa katika shambulizi la wapiganaji kutoka kundi la Kiislamu al-Shabab kutoka Somalia.
    Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa El Wak ambao uko katika eneo la mpaka kati ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya na Somalia.
    Polisi hao wanaaminika kuwa ndani ya gari lao wakishika doria katika barabara moja kabla yao kushambuliwa ghafla na wapiganaji hao
    Wawili kati yao walipoteza maisha yao huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.
    Shambulizi hili la leo limetokea takriban kilomita 5 pekee kutoka pahala ilikoshambulia basi ya usafiri wa umma mapema wiki iliyopita na kuua watu wawili.
    Vyanzo vya wapiganaji hao wa Al-Shabab pia vinadai kuwa walitekwa gari la kijeshi.
    Dai hilo halijathibitishwa.
    Hapo jana mtu anayeshukiwa kuwa mpiganaji wa Al Shabaab aliuawa alipokuwa akitega bomu la ardhini katika barabara hiyo yaLafey – El Wak.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI