• Seynation Updates

    Wednesday 23 December 2015

    KRISMASI YAPIGWA MARUFUKU NCHINI SOMALIA......



    Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.
    Mkurugenzi mkuu katika wizara ya maswala ya dini,Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Al Shabab.


    ''Maafisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yeyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiofungamana na dini ya Kiislamu.'' alisema Sheikh Mohamed.
    Al Shabab iliua wanajeshi 5 mwaka uliopita walipokuwa wakiadhimisha sikukuu ya Krismasi
    Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika AU iliyoko mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.
    Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kunyemelea.
    Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI