• Seynation Updates

    Sunday 31 December 2017

    MSIMAMO WA MAN U SI MZURI.. WAZIDI KUSHUSHWA NA KUCHANA MIKEKA


    Klabu ya Manchester United bado imeendelea kupata matokeo mabovu kwenye Ligi Kuu soka England baada ya jana kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Southampton


    Kwa matokeo hayo Manchester United ambayo ilikuwa nafasi ya pili kwa muda mrefu kwenye msimamo wa EPL imeshuka hadi nafasi ya tatu baada ya Chelsea jana kupata ushindi mnono.
    Wakati hayo yakitokea Manchester United imepata janga lingine kubwa zaidi kwa kuumia mchezaji wao tegemezi, Romelu Lukaku jana kwenye mchezo huo.
    Pia kupitia mtandao wa klabu hiyo umethibitisha kuwa mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimović kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kuanzia jana.
    Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kupata sare tatu mfululizo kwenye EPL na kupoteza mechi moja ya kombe la EFL.
    Matokeo mengine ya ya mechi za jana za EPL ni kama ifuatavyo.
     

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI