watu kumi wamekufa baada ya mlipuaji mabomu aliejitolea kufa kujilipua msikitini
Hata hivyo, Kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram la Nigeria limekua likifanya mashambulizi katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger tangu mwaka jana.
Mlipuaji huyo wa kujitolea kufa anaripotiwa kuwa alikuwa akishiriki ibada pamoja na waumini wengine pale alipojilipua , duru za usalama zimeliambia shirika la habari la AFP.
"Waumini 11 walikufa katika tukio hilo. ''Wa kumi na mbili alikufa jwa najeraha hospitalinihospital," kwa mujibu wa duru hizi.
Shambulio hili la bomu limekuja baada ya watu wawili kuuawa wakati wa usiku katika eneo hilo hilo katika shambulio lingine linaloaminiwa kutekelezwa na Boko Haram, kwa mujibu wa duru za usalama zilizokaririwa na AFP.
Wapiganaji kutoka na Nigeria wa kundi la Boko Haram wamekua wakiendesha mashambulizi upande wapili wa mpaka kaskazini mwa Cameroon.
Kampeni ya kundi hilo ya kuanzisha taifa la kiislam kaskazini mwa Nigeria imewauwa watu takriban 17,000 na kuwaacha wengine wapatao milioni tatu bila makazi.
|
Mlipuaji mabomu wa kujitolea kufa amewauwa watu kumi na kuwajeruhi wengine kwenye msikiti uliopo kaskazini mwa nchi ya Cameroon, kwa mujibu wa maafisa wa maene ya mbali ya kaskazini. Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment