Wengi miongoni mwa waliouawa wanadhaniwa kuwa ni polisi waliokuwa wakilinda kliniki.
Polisi wenye silaha huwalinda wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya kupooza nchini Pakistani ambao wamekua wakilengwa na mashambulio mabaya ya Islamic State miaka ya hivi karibuni.
Wanamgambo wa Islamic State wanapinga chanjo ya kupooza , wakisema ni mpango wa nchi za magharibi wa kufunga uzazi dhidi ya watoto wa Pakistani.
Pakistan na Afghanistan ni nchi pekee zilizosalia zenye visa vingi vya marathi ya kupooza.
Mlipuko wa bomu hilo ulitokea mapema subuhi wakati wahudumu wa kutoa chanjo na maafisa wa usalama walipokua wakiripoti kazini kabla ya kuelekea nje kwa mizunguko ya kutoa chanjo hiyo , amesema Sarfaraz Bugti, waziri katika jimbo la Balochistan ambalo Quetta ni mji mkuu wake.
Polisi katika eneo hilo wanasema kuwa mlipuko huo uliwauwa polisi 12, mwanajeshi mmoja na raia mmoja. Watu wapao 20 wamejeruhiwa.
No comments:
Post a Comment