Ligi kuu katika Shule ya Sekondari Anderlek Ridges` Ilifikia hatua ya Fainali katika Football, Netball na Basketball Mnamo tarehe 19-03-2016.Ilikuwa ni baada ya timu nyingi kuchezwa, katika mechi mbalimbali na pia katika makundi mbalimbali, ndipo Ilifikia Hatua ya Fainali ambapo hawa ndio walioingia hatua ya fainali:
- Form 3A & Form 4A _ - Football
- Form 3A & Form 4A_ - Basketball
- Form 2A & Form 4A_ - Netball
Katika Mchuano wa Mpira wa Miguu (Form 3A Vs Form 4A) Form 4A waliibuka na Ushindi wa Mabao 2-0. Hivyo kuwapelekea Kupata Zawadi nono ya Ng'ombe Mmoja na Mbuzi wawili.
Na pia katika Basketball Form 4A waliibuka na ushindi dhidi ya Form 3A, hatua hii iliwapelekea kupata zawadi nono ya Mbuzi.
Katika Netball Form 4A waliibuka na Ushindi dhidi ya Form 2A, hatua hii iliwapelekea kupata mbuzi.
No comments:
Post a Comment