Diwani
Isaya Mwita (CHADEMA) kupitia Vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar
es salaam, baada ya kuishinda CCM iliyopata kura 67, huku UKAWA
wakipata kura 84, ambapo kura 7 zili haribika.
Uchaguzi huo ulifanyika leo Machi 22 kuanzia majira ya saa 4.00 asubuhi katika ukumbi wa Karimjee.
Uchaguzi huo uliahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio
batili la mahakama lililowekwa na makada wa CCM, katika Mahakama Hakimu
Mkazi wa Kisutu.
No comments:
Post a Comment