• Seynation Updates

    Tuesday 5 April 2016

    MAGUFULI NA KAGAME KUKUTANA USO KWA USO RUSOMO-NGARA KESHO TAR 6/04/2016, WANANCHI KUSAFIRISHWA BURE KWENDA KUWAPOKEA MARAIS HAO>>>>

    [​IMG]


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ,kesho Jumatano,April 06 mwaka huu,2016 anatarajia kufanya ziara wilayani Ngara mkoani Kagera, kwa ajili ya kuzindua Daraja la Rusumo linalo unganisha nchi ya Tanzania na Rwanda pamoja na Jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha -(OSBP)la forodha.Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habarai, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi Honoratha Chitanda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli na kuongeza kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imejipanga kuwasafirisha wananchi watakaokosa usafiri ili kufanikisha mapokezi.Bi Chitanda amesema pia kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuhakikisha ziara ya Rais inakwenda vizuri bila kuingiliwa na dosari yoyote inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi wote kutii sheria.Katika ziara hiyo Rais magufuli anatarajia kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame atakaye shirikiana naye katika Uzinduzi wa Daraja la Rusumolinalounganisha nchi mbili za Tanzania na Rwanda.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI