Ni siku moja baada ya uongozi wa Chelsea ya Uingereza kutangaza kumpa mkataba wa miaka mitatu kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ambaye atajiunga na klabu yao mwishoni mwa msimu. Leo April 5 Antonio Conteameripotiwa kuwa, huenda akafungwa miezi sita.
Muendesha mashtaka Roberto Di Martino kutoka Italiaanaripotiwa na Sky Sports kuwa April 5 2016 ameendeleza shauri la Conte kutuhumiwa kwa upangaji wa matokeo ya mechi ya ushindi wa Siena wa goli 1-0 dhidi ya AlbinoleffeMay 2011 na sare ya goli 2-2 dhidi ya Novara May 2011.
Kama Antonio Conte atakutwa na hatia huenda akakutana na kifungo cha miezi sita, Conte alituhumiwa kujihusisha na upangaji wa matokeo msimu wa 2010-2011 wakati akiwa kocha wa klabu ya Siena ya Italia.
No comments:
Post a Comment