• Seynation Updates

    Sunday 25 September 2016

    DANGOTE KUICHUKUA ARSENAL?

    Ni kweli Arsenal inahitaji mtu kama Dangote aje achukue timu ili iende mbele ? Unadhani mwarobaini wa timu hiyo ni kupata mtu tajiri aimiliki ili ipate kununua wachezaji wazuri ipate mafanikio zaidi ?  Na makombe yaingie pale Emirate.


    dangote-orginal-sio-chibu

    ARSENAL YA SASA IKOJE

    Arsenal ya sasa iko vizuri lakini kuna ubahili mkubwa labda wengi hawajui tatizo haswa nini nini hadi Wenger hachukui wachezaji wenye viwango vya dunia, lawama imekuja kwa Wenger kwa kuwa ndiyo anaonekana kila siku lakini kuna kitu kiko nyuma yake. Alisher  Usmonov anatamani awe anahisa kubwa ili awe anaweza kusema chochote pale Arsenal, kuna mtu anaitwa Stan Kroenke yeye ndiye chanzo cha ubahili wa Wenger japo Wenger anahusika pia.

    ARSENAL YA DANGOTE

    Kama kweli atachukua  timu hiyo basi itakuwa heri sana kwa kuwa Arsenal inahitaji mtu mwenye maamuzi na anatamani kuipa kitu Arsenal anaipenda timu hiyo hivyo kama inawezekana apate timu japo anatakiwa ajiangalie mara mbili kwa utajiri wake. Lakini pia jiulize ni kweli ataweza kuisimamia timu hiyo kwa kuwa mimi si mtalaamu wa fedha nisifike huko naangalia  tu anaweza kupambana na kina Abromovich.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI