• Seynation Updates

    Tuesday, 29 May 2018

    Hili hapa Tamko la Azam Fc Kwenye Msimu Huu

    Klabu ya soka ya Azam FC ambayo jana imefanikiwa kumaliza ligi kuu msimu wa 2017/18 katika nafasi ya pili baada ya kuifunga Yanga, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo Abdulkarim Amin amesema mashabiki ndio chanzo cha matokeo hayo.



    Akiongea na East Africa Television, Abdulkarim amesema wao kama Azam FC wanawashukuru mashabiki kwa kuwa nao pamoja kwa msimu mzima na mafanikio ya kumaliza katika nafasi ya pili ni kutokana na wao kuwapa nguvu hata pale wachezaji walipohisi ugumu wakiwa uwanjani.
    ''Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki mmekuwa pamoja na timu kila sehemu mnapoweza hakika nyinyi ni chachu ya kumaliza nafasi ya pili'', amesema.
    Mbali na hilo Abdulkarim amewaomba mashabiki kuendelea kuwapa 'support' wachezaji na benchi la ufundi kwa ujumla huku akiahidi makubwa msimu ujao kutokana na namna ambavyo uongozi umejipanga ili timu ifanye vizuri.
    Azam FC msimu huu ilikuja na mpango wa kuondoa wachezaji wenye umri mkubwa na kuwekeza zaidi kwa vijana ambapo iliwaondoa Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, John Bocco na wengine kuwatoa kwa mkopo kama Mudathir Yahya.
    CREDIT : EATV
    Usikose habari zaidi Tufuatilie Instagram @seynation na INSTALL APP YETU BOFYA HAPA

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI