KWAMBA TAREHE 04.12.2016 MAJIRA YA SAA 00.02HRS USIKU KATIKA MTAA WA IGOGO TANESCO WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MLINZI WA KAMPUNI YA ULINZI IITWAYO MAIKA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA MICHAEL BONIPHACE @ UDILIKA MIAKA 38, MKAZI WA KISHILA – BUHONGWA ALIPORWA SILAHA AINA YA SHORT GUN YENYE NAMBA CT.0910 NA RISASI SITA NDANI YA MAGAZINE AKIWA LINDONI BAADA KUVAMIWA NA WATU WAWILI WANAOZANIWA KUWA NI MAJAMBAZI.
INADAIWA KUWA MLINZI HUYO ALIKUWA KWENYE LINDO LA GHALA LA RTC LILILOKODIWA NA KAMPUNI YA MOHAMED ENTREPRISES LINALOHIFADHI BIDHAA MBALIMBALI ZA CHAKULA, ALIVAMIWA NA WATU WAWILI ASIO WAHAFAHAMU KISHA WAKAMPIGA NA KITU KIZITO KICHWANI NA KUPOTEZA FAHAMU NA KUPORWA SILAHA AINA YA SHORT GUN IKIWA NA RISASI SITA NDANI YA MAGAZINE, INAONEKANA MLINZI HUYO ALIZEMBEA NA WEZI HAO KUPATA UPENYO WA KUTENDA UHALIFU HUO.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WANAODAIWA KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILO, UPELELEZI NA MSAKO MKALI WA KUSAKA SILAHA HIYO BADO UNAENDELEA, MAJERUHI AMEPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA TAARIFA POLISI MAPEMA MAHALI AMBAPO SILAHA HIYO IMEFICHWA KABLA HAIJALETA MADHARA KWA WANANCHI, LAKINI PIA ANAWASIHI WALINZI WA MAKAMPUNI YA ULIZNI NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA KUWA MAKINI KATIKA KIPINDI HIKI PINDI WANAPOKUWA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment