U Heard ya Soudy Brown ya December 21, 2016 kupitia XXL ya Clouds FM iko na story kuhusu mastaa wa kundi maarufu la muziki wa Bongo Flava YA MOTO BAND kutokuwa na maelewano mazuri kati yao na inaelezwa kuwa hivi karibu muimbaji Aslay aliamua kuondoka kwenye nyumba waliyopangishiwa maeneo ya Tabata na kuamua kuishi mwenyewe na mke wake pamoja na mtoto wao.
Soudy Brown amezungumza na meneja wa kundi hilo aitwaye Chamboso ambaye ameeleza kuwa kuondoka kwa Aslay kwenye nyumba hiyo haina maana kwamba wamegombana kwenye kundi lao ila ni maamuzi yake mwenyewe na inawezekana sababu ni kuwa na familia hivyo anataka kuwa huru.
“Hakuna mvutano bwana, kwani kama Aslay kahama Tabata ndio kuna mvutano? hakuna chochote na show zinaendelea kama kawaida hata juzi kwenye uzinduzi wa band ya taarab ya TMK walikuwepo na waliimba kila pamoja na wako pamoja mimi ni meneja wao nashinda nao kila siku nakuhahakishia hakuna tatizo” – Meneja Chambuso
No comments:
Post a Comment