Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Arusha Bw Khalifa Lihundi anashikiliwa na polisi kituo cha Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa tuhuma za kuandika habari za zinazodaiwa kuwa ni za uchochezi.
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV mkoani Arusha, Khalfan Lihundi.
Bw Lihundi amekamatwa jijini Arusha majira ya saa nane mchana na askari anayedaiwa kutumwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw Alexsander Mnyeti kama anavyoeleza Bw Basili Elias ambaye alishuhudia tukio hilo.
Akizungumzia suala hilo mpiga picha wa Bw Khalifand Lihundi Bw Deogratius Kassamia amesema habari inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ilikuwa ni ya malalamiko ya wananchi juu ya tatizo la maji.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha Bw Cloud Gwandu pamoja na kulaani kitendo hicho amesema hatua hiyo haikubaliki kwani haikufuata taratibu.
No comments:
Post a Comment