Tukiwa tunamsubiria Diamond kwenda kuiwakilisha Tanzania akiwa kama msanii ambaye ni miongoni waliochaguliwa kwenda kutumbuiza kwenye ufunguzi wa mashindano ya AFCON huko nchini Gabon, Waziri wa Habari, Utamaduni, wasanii na michezo Nape Nnauye amemkabidhi Bendera ya Taifa Diamond kama uwakilishi.
Akizungumza wakati wakumpatia Bendera hiyo nyota huyo wa Bongo fleva Diamond platnumz, Nape Nnauye alifunguka na kusema kwamba Tanzania imepata nafasi ya kipekee kupitia sanaa ya muziki kwa kuungana na wasanii watatu Afrika kuunda wimbo maalumu ambao utatumika katika mashindano hayo ya Afcon 2017 ambayo yanatarajiwa kufunguliwa january 14.
“Mashindano ya Afcon ni mashindano makubwa, yataangaliwa na bara zima la Afrika, lakini pia yataangaliwa na dunia nzima, amepata fursa ya kupeperusha bendera ya nchi yetu duniani, na mimi naamini fursa hii ataitumia vizuri na itakuwa msingi na ufunguo kwa yeye kufanya vizuri kwenye tasnia hii kwenye nyanda za kimataifa, shughuli hii ni usibitisho kwamba sanaa ya nchi yetu inakua na ndio maana imepata fursa ya kuonwa na kupata fursa ya kwenda kutumbuiza kwenye onesho hili muhimu,……hii inanonyesha namna sanaa yetu inavyozidi kukua siku hadi siku, Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii wa tatu Afrika watakao tumbuiza live wimbo maalumu utakao tumika katika mashindano hayo..” Alisema Nape.
Hata hivyo Diamond platnumz alifunguka na kuwataka waTanzania wajivunie hatua aliyofikia kwamba kamwe hatowaangusha akiongeza pia kuwataka wadau wengine wajitokeze kwa wingi kuwadhamini wasanii wachanga.
“Kwanza kabisa nimshukuru Mh Waziri wa Habari, michezo, sanaa na burudani kwa kuhaikisha kwamba anakuwa bega kwa bega na tasnia anazoziongoza na kuhaikisha kama vijana wake…..nawapongeza Serikali hata kwa kumteua….vilevile namshukuru kaimu mkurugenzi wa kutoka DSTV na kampuni nzima ya DSTV kwa kuweza kuwa nao pia mstari wa mbele…” Alisema Diamond.
Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Salum Salum ametoa tiketi sita za kwenda na kurudi kwa vijana wa WCB kwenda Gabon kwa ajili ya kuhakikisha kwamba uzinduzi huo unafanyika sawia.
Kilichobaki ni kwa Watanzania sasa kujivunia kwa hatua ya muziki wetu wa Bongo fleva ulipofikia na unapozidi kuendelea kukua kila kona ya Dunia.
Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye FACEBOOK na INSTAGRAM @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.
No comments:
Post a Comment