• Seynation Updates

    Wednesday 11 January 2017

    ALICHOKISEMA PROFESSOR JAY JUU YA MBUNGE ALIYEHUKUMIWA JELA MIEZI SITA.

    Baada ya mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali na Dereva wake, John Kibasa kuhukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini kwa kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi mwaka 2015, Professor Jay ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi ameumizwa na kitendo hicho.
    Kupitia ukurasa wa facebook wa Professor ameandika:
    Wanadhani wanatutisha ili tuogope Na kurudi nyuma, Hawajui kuwa WANATUKOMAZA Na kutuongezea Ujasiri zaidi wa Kuendeleza Mapambano. Ipo Siku TUTAELEWANA TU na Jela tutaona kama tumekwenda DISCO! Congratulations Mpiganaji @mh.lijualikali Hatujui kesho ni zamu ya nani ila WE ARE VERY READY!! TRUST ME. ALUTA CONTINUA.
    Mbunge huyo wa Kilombero atatumikia adhabu ya miezi 6 jela na baada ya kumaliza hukumu hiyo na kuachiwa huru ataendelea na kazi yake ya ubunge kama kawaida kwani sheria inasema mbunge akifungwa jela zaidi ya miezi sita kwa kosa lolote basi atapoteza nafasi yake ya ubunge.

    SOURCE: BONGO5


    Ili ujue kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu kwenye   FACEBOOK na  INSTAGRAM  @seynation ili niwe nakutumia kila kinachoonifikia.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI