• Seynation Updates

    Sunday 12 February 2017

    PICHA: NGAYA YAWA WATEJA KWA YANGA.


    Baada ya kuishia hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho barani Afrika msimu uliyopita, Mabingwa wa Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans wamecheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza wa Club Bingwa barani Afrika ugenini dhidi ya Ngaya Club ya Comoro Jumapili ya February 12.
    Yanga waliingia kucheza dhidi ya Ngaya wakiwa na tahadhari kubwa kwa mujibu wa kocha wao msaidzi Juma Mwambusi, hiyo inatokana na rekodi ya timu hiyo ambayo kuanzia mwaka 2016 hadi sasa ilikuwa haijapoteza mchezo wowote katika michezo ya 32 wakiwa wametoa sare mechi 6 za ugenini pekee.
    Kikosi cha Ngaya licha ya kujumuika na wachezaji 5 wakimataifa, watatu wakitoka Ivory Coast na wawili wakitokea Madagascar, wamekubali kipigo cha goli 5-1, magoli ya Yanga yakifungwa na Justine Zulu, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko, goli pekee la Ngaya limefungwa na Saidi Anifane.
    Ngaya pia ambao watarudiana na Yanga baada ya wiki moja uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wanawachezaji wawili wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Comoro ambayo ipo nafasi ya 141 katika viwango vya FIFA ikilinganishwa na Tanzania iliyopo nafasi ya 158.

    Jiunge na Seynation Media.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI