• Seynation Updates

    Wednesday 29 March 2017

    Sababu 10 zinazofanya ushauriwe kukumbatiana sio chini ya mara 8 kwa siku.



    Kitendo cha kukumbatiana sio tu kinaleta upendo na kuileta jamii pamoja bali kina faida kubwa za kiafya na kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa, watu hushauriwa wakumbatiane sio chini ya mara 8 kwa siku nimekusogezea hapa  faida 8 za kukumbatia.

    1- Husaidia kupumzisha ubongo.

    Kumkumbatia mtu unaye mjali au kumpenda  kunasaidia ubongo kuzalisha homoni inayojulikana kama OXYTOCIN  homoni hii husaidia ubongo kufika level kubwa ya kupumzika, pia homoni ya OXYTOCIN  humsaidia mwanamke mwenye ujauzito kuzaa kwa usalama zaidi kwani hufanya mfumo wa uzazi kupanuka.

    2- Husaidia mwili kupambana na magonjwa.

    Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wengi hasa wazee wanaokumbatiwa mara nyingi huwa na asilimia chache za kukumbwa na magonjwa kuliko wale ambao hawakumbatiwi, hivyo watu hushauriwa kukumbatia wazazi wao kwani hii itawasaidia miili yao kuzalisha kinga ya kupambana na magonjwa.

    3- Kukumbatiana husaidia kupunguza maumivu.


    Madaktari hushauri kukumbatia wagonjwa wetu kwani kitendo hiko kidogo kinasaidia ubongo kuachia homoni  inayojulikana kama  endorphins ambayo husaidia kufunga njia zote katika ubongo ambazo hutuma taarifa ya kuwepo kwa maumivu kwenye mwili.

    4- Husaidia watu kuwa na mood nzuri.

    Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wenye hasira au mood mbaya kila siku huzalisha homoni  chache sana za Dopamine na Serotonin ambazo zinasaidia kufanya ubongo kuwa na uchovu na kukosa furaha hivyo kukumbatia mtu unaye mpenda inasaidia kuzalisha homoni hizi kwa wingi.

    5- Kukumbatiana huongeza ufahamu kwenye ubongo.

    Watu wanashauriwa kukumbatia watu wenye uzito wa kuelewa mambo kwa haraka hasa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa kama  Autism na Dementia  kwani kitendo hiki husaidia ubongo kuzalisha homoni ya oxytin inayosaidia ubongo kuelewa jambo kwa haraka na kutatua maswali magumu.

    6- Hupunguza  msongo wa mawazo .

    Kukumbatiana kuna saidia kupunguza uzalishaji wa homoni inayoitwa  Cortiso ambayo husaidia ubongo ku-relax, homoni hii ikizalishwa kwa wingi kwenye ubongo wa mwanadamu basi mtu huyo hutawaliwa na mawazo hasi yanayopelekea msongo wa mawazo.

    7- Humsaidia mtu kupunguza hofu .

    Tafiti iliyofanywa na  Psychological Science Journal imeelezea umuhimu wa kukumbatia mtu mwenye hofu kwani inasaidia ubongo kupuuza taarifa hasi zinazotumwa kwenye ubongo pia husaidia mtu kuzalisha homoni zitakazomfanya ajiamini.

    8- Huepusha mtu kupata magonjwa ya akili.

    Kukumbatiana kunasaidia kuzalisha kwa homoni ya Dopamine ambayo uzalishwaji wa homoni hii husaidia ubongo kupambana na magonjwa ya akili kama Depression, Bipolar pamoja na Dementia  pia homoni hii inasaidia mtu kujiamini na kuwa mkweli.

    9- Husaidia kuepusha magonjwa ya moyo .

    Utafiti uliofanywa  North Carolina umesema kuwa watu ambao hawajaonana na wapenzi wao kwa muda mrefu mapigo ya moyo huongezeka kwa mapigo 90 ya moyo kwa dakika na hali hii sio nzuri kwani binadamu  mwenye afya imara hupata mapigo 40 kwa dakika moja.

    10- Husaidia kupumzisha misuli ya mwili .

    Kukumbatiana kunasaidia kupumzisha misuli ya mwili ambapo watu wengi wanapokumbatiana hulegeza misuli yote iliyokaza na kusaidia mwili kupumzika ndio maana wazazi wengi hushauriwa kukumbatia watoto wao  wanapo amka asubuhi na kabla hawajalala.
    Chanzo: millardayo.com

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI