• Seynation Updates

    Thursday 23 March 2017

    Viongozi, mastaa watoa maoni yao kufuatia Nape kupokonywa uwaziri, wengi wamuita ‘shujaa’.

    Alhamis hii jua limechomoza likiambatana na mshtuko mkubwa kwa wananchi wengi wa Tanzania.
    Mshtuko huo umetokana na taarifa ya mheshimiwa Nape Nnauye kupokonywa nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii imekuwa habari yenye mpasuko mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nape ameonekana kuwa mtetezi muhimu wa vyombo vya habari kufuatia kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha nzito.
    Ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokea ripoti toka kwenye kamati aliyokuwa ameiteua kufanya uchunguzi wa tukio hilo, Nape ameondolewa na kuacha sintofahamu kubwa kwenye mkasa huo.
    Mastaa, viongozi na wananchi wametoa maoni yao ambao mengi yanafanana – hawajependezwa na kilichotokea huku wengi wakimwelezea Nape kama shujaaa.
    Haya ni baadhi yao:
    Zitto Kabwe
    Nimezungumza na mbunge wa Mchinga @Nnauye_Nape na kuthibitisha kuwa Ni Kweli ameondolewa kwenye Uwaziri. Nape ni Shujaa wa kizazi chetu
    Irene Kiwia
    The key resource of ordinary citizens is numbers. And justice will reign on earth and truly will the voice of the people be the voice of God. When there is true awakening of the people, in numbers, it forms the real and conscious public opinion.
    B12
    Nitakua naota eti……. Ngoja nilale tena then niamke! Maana hii si mara ya kwanza kukutana na ndoto mbaya ya kutisha!!
    Nchakalih
    Kaka @Nnauye_Nape nakushukuru kwa kunipa mfano wa kutumia kumfundishia mwanangu zion somo la uzalendo! HISTORY will JUDGE you RIGHT!! 👊👊
    Halima Mdee
    Naamini ni UZUSHI!!
    Edo Kumwembe
    Sidhani kama Nape anajali…alilitafuta hili kwa nguvu zote…sidhani kama anajali

    Bonge la Nyau
    Huyu ni shujaa wangu……
    Wema Sepetu
    We will Surely Miss U as Our Minister… Tulishakuzoea. Such a way to start Your Morning.. Lets wait for what’s NEXT…. This Is Tooo Much Jamani. This Country Be Full of Surprises Nowadays…. Smh.. Never Knew Nchi ina MaRais wawili… Now I know…. Smh…
    Idris Sultan
    Raisi akashika Jiwe na Almasi akavipimaaaaaaaa aksema embu katupeni almasi ina’ngaa kijinga jinga tu nimeiambia ing’ae kwani.
    Madee‏ 
    Sad newz😭😭
    Masoud Kipanya
    Haya ni mawazo yangu… Ningekuwa @Nnauye_Nape ningekaa KIMYA kabisa
    Diva
    Nimepata mshtuko wa mwaka 🤥. Kama Kijana Mpenda Haki na Mpenda Maendeleo na Ninaejitegemea Nimepata Mshtuko wa Mwaka , Nimejiuliza maswal Kwa uchungu Chozi limetoka 🤥🤧
    Peter Msigwa
    Kwa Magufuli bashite ni mhimu na ni bora kuliko Nape ndani ya chama na serikali! Hongera JPM!
    Mwana FA
    (Alitweet muda mfupi kabla ya habari za kuondolewa uwaziri (Toka mwanzo kabisa wa haya maswahibu,kaka yangu @Nnauye_Nape anaonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa..kisiasa na kibinadamu. Anajua umuhimu wa kufanya ‘vita’ dhidi ya mambo yasiyo sahihi kwa jamii bila dhulma na ukiukwaji wa sheria,na hayumbi kwy kusimamia ukweli.
    NA HARINGI 😀..SALUTE kaka @Nnauye_Nape …najivunia kusema nakujua,ubarikiwe ndugu yangu)
    Baada ya habari hiyo kufahamika alitweet: Aisee..
    Aika
    Its not dictactorship its being a coward #JustSaying running frm people challenging u 🇹🇿

    Jiunge na SeyNation

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI