Katika mchezo huo ambo Yanga haikukumbana na ushindani wowote na kufanikiwa kutawala mchezo kwa zaidi ya asilimia 70 kwa 30, imeanza kujipigia katika dakika ya 11 kupitia kwa Geofrey Mwashiuya, kabla ya Mzambia Obrey Chirwa kupachika la pili dakika ya 22, na Kiluvya kupata bao lao dakika ya 40 kupitia kwa Edgar Mfumakule, ambapo hadi mapumziko Yanga ikaondoka ikiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili, Chirwa ambaye alikuwa na mchezo mzuri zaidi siku ya leo, alifanikiwa kuongeza mabao mawili, dakika ya 48 na dakika ya 70, huku Juma Mahadhi akipiga la 5 dakika ya 74, kabla ya Chirwa tena kuhitimisha sherehe ya mabao dakika ya 87 kwa kufunga bao la sita, likiwa ni bao lake la nne katika mchezo wa leo na kuondoka na mpira.
Baada ya matokeo hayo sasa Yanga itakutana na Wajelajela, Tanzania Prisons katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya robo fainali kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa leo.
No comments:
Post a Comment