• Seynation Updates

    Saturday, 22 April 2017

    ATEMBEZWA Nusu UCHI Na Kisha Kulazimishwa Kula Kinyesi kwa Kosa la Kumtukana Mama Yake





    Wanawake wa kijiji cha Kisungamile kilichopo katika Kata ya Matai wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wamemwadhibu Vitus Nyami (26) kwa kumtembeza nusu uchi na kulazimisha kula kinyesi cha ng’ombe kwa kosa la kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni.

    Aidha wanawake hao walitumia mfuko wa ‘salphate’ kufunika sehemu za siri za kijana huyo kisha wakaanza kumtembeza mitaani kijijini  humo huku wakiimba nyimbo za kabila la Kifipa wakilaani tabia ya kijana huyo ya kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni kila kukicha .

    Walidai kukasirishwa na tabia ya kijana huyo wa kiume kumtukana mzazi wake wa kike matusi ya nguoni, hivyo walilazimika kumfunga kamba na kumtembeza mitaani kijijini humo akiwa nusu uchi.

    Mwenyekiti wa kijiji cha Kisungamile, Didas Musa alikiri kutokea kwa mkasa huo juzi ambapo mtuhumiwa huyo alitembezwa mitaani kwa saa sita kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

    Akifafanua alisema kuwa licha ya adhabu hiyo ya kutembezwa nusu uchi mitaani na kucharazwa viboko 15, pia ameamriwa kulipa mbuzi mmoja, unga wa sembe debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.

    “Adhabu hii kwa kijana hutolewa na akina mama ambapo mimi kama kiongozi kazi yangu ni kuibariki tu,” alisisitiza . Mkazi wa kijiji hicho, Obedi Mwanakatwe alisema kijana huyo amekuwa akimtukana mama yake mara kwa mara , tabia ambayo imekuwa ikiwachukiza akinamama kijijini humo ambapo waliandamana na kumkamata kijana huyo .

    “Baada ya akinamama hao wenye hasiri kumkamata kijana huyo walimpeleka kwenye shimo lililojaa kinyesi cha ng’ombe kisha wakampaka kinyesi hicho mwili mzima wakiwa wamechanganya na unga wakisaidiwa na wanaume, walimtembeza uchi kijana huyo mitaani kijijini humo,” alieleza.

    Stela Tenganamba alisema baada ya kumtembeza kwa muda mrefu waliamua kumlisha kinyesi cha ng’ombe na kumpaka mwili mzima sambamba na kumroweka kwenye matope.

    Adhabu hiyo iliwekwa enzi za mababu zao , ambapo mtu yeyote anayetukana matusi hadharani huchukuliwa hatua hiyo sambamba na kulipishwa ng’ombe mmoja, mbuzi, unga debe moja na mafuta ya kupikia lita moja.

    Akifafanua alisema kuwa baada ya kutembezwa mitaani akiwa uchi hupelekwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambaye hutoa adhabu kulingana na akinamama watavyoona inafaa

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI