JERRY MURO: "Yanga kuna majungu,Yanga kuna watu wanapenda wafanye vitu vyao,Yanga kuna wanafiki, wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka,Yanga kuna watu wazuri sana, Yanga kuna watu wenye akili, Yanga kuna watu kwenye msaada wa kweli, Yanga kuna watu wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama TP Mazembe watu wote hao wapo Yanga"
Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali watoto wake,yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo,Yeye mwenyewe kuvaa vest safi havai maisha yake yamemshinda''
Mungu anasema unapojipenda nafsi yako wewe mpende na jirani, kaka kama MTU kashindwa kuendesha familia yake kamwe hawezi kuendesha Yanga''