Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dr. Josephat Gwajima jana alijitokeza hadharani mbele ya waumini wa kanisa lake na kumtaka Halima Mdee Mbunge wa CHADEMA kumuomba radhi Spika wa Bunge Job Ndugai kwa maelezo kuwa alimtukana. Gwajima alisema, kama hatafanya hivyo, basi ataitumia Jumapili Ijayo 'kumchapa' Hadharani
Kutokana na madai hayo, Halima Mdee amejitokeza hadharani na kumjibu Gwajima
"Namuheshimu sana Mch. Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.
"Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO."
No comments:
Post a Comment