Kioja! Mastaa wawili wasioishiwa vituko wanaounda Kundi la Muziki la Scorpion Girls, Baby Madaha na Isabela Mpanda, wikiendi iliyopita waliwaacha watu midomo wazi baada ya kujiachia kimahaba kama mtu na mpenziwe.
Baby Madaha na Isabela walilishana keki kwa staili ya njiwa ‘kugusanisha midomo’ ikiwa ni kwenye sherehe ya bethidei ya Isabela iliyofanyika katika Hoteli ya Belinda iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.
Akizungumza katika ishu hiyo, mmoja wa wahudhuriaji ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema tukio hilo ni la kushangaza kwani linaashiria kuna kitu kingine nyuma ya pazia kwa wasanii hao marafiki wa muda mrefu.
“Kiukweli Isabela na Baby wamenishangaza sana, maana kulishana huko keki kama mtu na mpenzi wake inaashiria kuna kitu nyuma ya pazia, inawezekana wenzetu ni wapenzi wa jinsia moja (wasagaji), maana siyo kwa ukaribu huo tena hadharani, hawaogopi hata watu tuliopo hapa jamani, kweli dunia imevaa koti,” alisema mmoja wa wahudhuriaji.
Alipoulizwa Isabela kulikoni kulishana keki na Baby kama wapenzi, alisema jambo hilo ni la kawaida tu kwa kuwa ni marafiki na hakuna kitu kingine chochote kinachoendelea kati yao. “Sisi ni marafiki na tumeshakuwa kama ndugu hivyo kulishana keki hivi kwa mdomo ni upendo tu na hakuna mambo ya usagaji kama wengi wanavyohisi wala nini,” alisema Isabela.
CREDIT: Udaku Special