• Seynation Updates

    Thursday, 25 January 2018

    Mawakili watatu wa Sugu, wajiengua




    Mawakili wa utetezi katika kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga wamejiondoa kutokana na kutokuwa na imani na muenendo wa kesi hiyo na kuwataka watafute Mawakili wengine.

    Uamuzi huo wa Mawakili hao watatu ambao ni Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo umetolewa leo (Alhamisi) baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Michael Mteite, kugoma kujitoa katika usikilizaji wa kesi hiyo kama walivyotaka washtakiwa hao hapo awali kwa madai hawana imani nae.
    Aidha, Hakimu Mteite alisema kuwa miongoni mwa sababu za yeye kuendelea na kesi hiyo ni kuwa Mahakama inayojukumu la kutoa dhamana au kutotoa kwa jinsi itakavyoona pia kuhusu ugumu wa kesi hiyo alikua anaamanisha ni kwamba inamvuto huku akidai hataweza kuendesha kesi hiyo kwa kumuogopa mtu kwa maana alikula kiapo.
    Hata hivyo Wakili wa Jamhuri Joseph Pande aliiambia Mahakama kwamba Mawakili wa utetezi kujitoa kwenye kesi hiyo ni jambo la kawaida kwa kuwa wana sababu zao mbalimbali ambazo hawawezi kuzizungumza licha ya kuwa awali upande wa utetezi walikubali kuendelea na kesi hiyo.
    Pamoja na hayo, Sugu na Masonga waliomba Mahakama kutoa (kuwapa) muda wiki mbili ili waweze kutafuta Mawakili wengine wawasimamie kesi yao hiyo kwa sababu wapo rumande hivyo itawachukua muda mrefu kujipanga na kuwatafuta na endapo itashindikana basi watajitetea wenyewe.
    Kutokana na ombi hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahamaka ya Hakimu Mkazi Mbeya Michael Mteite aliwakubalia washtakiwa hao  matakwa yao na kuiharisha kesi hadi Februari 8 mwaka huu ambao itasikilizwa kwa mara nyingine.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI