• Seynation Updates

    Wednesday, 17 May 2017

    "Nitamnyoosha Afande Sele Aache Kidomodomo" Harmorapa


    Msanii Harmorapa amefunguka na kumkumbusha Afande Sele kuwa hata yeye heshima aliyonayo sasa kwenye muziki haikuja tu kwani hata yeye alianzia chini kama ambavyo yeye ameanzia na baadaye ndiyo akawa msanii mkubwa.

    Harmorapa amefunguka hayo kufuatia rapa huyo mkongwe kumdiss na kusema anabebwa tu na P Funk Majani, hivyo Harmorapa anasema yeye hataki kuongea sana bali anaaziachia kazi zake zimnyooshe Afande.

    Ikumbukwe Afande Sele siku za hivi karibuni amekuwa mara kwa mara akiingia katika kujibishana na kutofautiana na wasanii mbali mbali kutokana na mitazamo yao.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI