• Seynation Updates

    Wednesday, 17 May 2017

    JACK Wolper “Kwenye Maisha Yangu Sijawahi Kuachwa, Sina Kabisa Record Hiyo"

    Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kuizungumzia ishu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize.

    Muigizaji huyo amedai hana msongo wa mawazo kutokana na tukio hilo huku akidai hajaachwa kama baadhi ya watu kwenye mitandao wanavyodai.
     “Kuachwa ndio nini? kweli usilolijua ni kama usiku wa giza,” Wolper alikiambia kipindi cha U Heard cha Clouds FM. “Kwenye maisha yangu sijawahi kuachwa, sina kabisa record hiyo sema sitakagi kufanywa mjinga. Yeye kama amezungumza ishu ya kuachana na mimi, mimi sitaki kulizungumzia kwa sababu na mambo yangu mengi ya umuhimu nafanya,”

    Harmonize hivi karibuni alifunguka na kuweka wazi kwamba hayupo tena kwenye mahusiano ya mrembo huyo kutoka tasnia ya filamu huku akishindwa kueleza sababu.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI