• Seynation Updates

    Monday 26 June 2017

    HAKIELEWEKI YOUNG KILLER NA NEY WA MITEGO...NI BIFU KALIIII

    Nay Wa Mitego Ampiga Dongo Young Killer baada Ya Kuisikiliza ‘True Boya’?

    Baada ya Nay wa Mitego kuachia wimbo wake mpya ‘Moto’ambao ndani yake amewachana wasanii mbalimbali akiwemo rapa Young Killer Msodoki na baadaye Young Killer kuamua kumjibu kupitia wimbo ‘True Boya’, Nay amerudi kivingine tena.
    Rapa huyo ambaye ana tabia ya kuachia nyimbo za kuwachana wasanii wenzake, amepost video ya wimbo wake huo kupitia mtandao wa Instagram nakutuma maneno ambayo yanadaiwa kwenda kwa rapa huyo kutoka Mwanza.
    “Thanks @cloudsfmtz Muziki Sio kuandika tu Mistari, Nidhamu itakufanya Ufike Mbali. #Moto🔥 Bonyeza Link kwenye Bio☝🏾️apo Juu Kusikiliza,” aliandika Nay wa Mitego Insta.
    Hata hivyo mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii wamedai alichokifanya Young Killer Msodoki ni kitu sahihi kutokana na rapa huyo kuzoea kuwachana wasanii wenzake.
    Kupitia wimbo ‘Moto’ ya rapa huyo alimchana Young Killer kwamba ameshindwa muziki na anatakiwa kurudi nyumbani kwao Mwanza.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI