Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na serekali ya Algeria zinaeleza kwamba serekali hiyo imeamuwa kusimamisha mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter baada ya kugundua na kuthibitisha wizi wa mitihani ya kitaifa nchini humo na kusambazwa kwa zaidi ya wanafunzi laki 550,000 kupitia mitandao ya Facebook na Twetter kabla ya mitihani hiyo kufanyika.
Uamuzi huo ulichukuliwa na serikali hiyo siku ya Jumamosi usiku.
Serikali hiyo baada ya kugundua hilo iliamua kuahirisha mitihani hiyo ya kitaifa na kuamuru mitandao ya kijamii ifungwe mpaka pale ambapo itakapotungwa mitihani mingine mipya.
Source: TRTWorld and agencies
No comments:
Post a Comment