• Seynation Updates

    Friday, 1 December 2017

    Neymar na Edison Cavanni “kimenuka” tenaa



    Tangu Neymar ajiunge na PSG mambo yamebadilika sana, tofauti na upendo aliokuwa akiupata Barcelona hivi sasa mchezaji huyo amekuwa akiandamwa na majanga ambayo tayari yanatajwa kumkosesha amani PSG.
    Kati ya watu ambao wamekuwa wakimkosesha amani Neymar tangu ajiunge PSG ni mshambuliaji wa Uruguay Edison Cavanni ambaye wakati Neymar anatua tu PSG walianza kugombana kuhusu suala la upigaji penati.
    Baadaye Neymar na Cavanni  walionekana kuwa sawa na maisha yakawa yanaendelea kama kawaida ndani ya klabu hiyo, lakini wakati watu wakifikiria jambk hilo limekwisha, usiku wa jana wawilo hao kwa mara nyingine walitibuana.
    Katika mchezo zidi ya Troyes usiku wa jana kulitokea mpira wa adhabu na kama kawaida Cavanni alitaka kuuchukua mpira huo ili kuupiga lakini Neymar naye alitaka kuupiga mpira huo.
    Nahodha wa PSG Thiago Silva na kiungo Javier Pastore walionekana kusogea karibu na wachezaji hao ili kujaribu kupunguza majadiliano kati ya wawili hao na baadaye Neymar alionekana akiondoka katika eneo hilo.
    Baada ya tukio hilo inadaiwa kwamba Neymar aliomba msamaha katika vyumba vya kubadilishia nguo huku kocha wa klabu hiyo Unai Emery akisisitiza kwamba mpigaji tuta katika klabu hiyo ni Edison Cavanni.
    Ugomvi unaoendelea PSG unaweza kuwa furaha kwa Real Madrid ambao wanaonekana kufuatilia kwa ukaribu sakata la Neymar, na watabiri wa mambo tayari wanaamini kwamba kati ya Neymar na Cavanni mmojawao lazima ampishe mwenzake.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI