• Seynation Updates

    Tuesday, 28 November 2017

    KUAPISHWA KWA KENYATTA KUMEGEUKA KILIO KWA WANANCHI WA KENYA

    Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Mamia ya Watu Karasani

    Polisi wametumia mabomu ya machozi kudhibiti mamia ya watu waliokuwa wanataka kuingia kwa nguvu kwenye uwanja wa Kasarani ambako zinafanyika sherehe za kuapishwa Rais Uhuru Kenyatta.

    "Haki yetu, Haki Yetu," walipiga kelele watu hao ambao wengi wao walikuwa wamevalia nguo za rangi za chama tawala cha Jubilee walipokuwa wakisukumana kutaka kuwapita polisi.

    Maofisa wa polisi waliwazuia watu hao wakawapiga baadhi na kuwaacha wakiwa majeruhi. Baadhi walipata tiba ya huduma ya kwanza wakati walioumia zaidi walisafirishwa hadi Hospitali ya Taifa ya Kenyatta.

    Polisi walionekana wakiwakimbiza baadhi ya watu wakati wengine walipita kwa nguvu kwenye milango.

    Kulikuwa na farasi na magari ya kubeba wagonjwa. Ulinzi ni mkali na wahudhuriaji wote lazima wapekuliwe kuingia ndani ya uwanja huo ambamo wageni kutoka nchi 20 – wakuu wa nchi au mawaziri – wamehudhuria.

    Hata hivyo, kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga, aliyesusia uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 amesusia sherehe hizo na badala yake alikuwa amepanga kuhutubia mkusanyiko mwingine mkubwa eneo la Jacaranda kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wao waliouawa wakati wa maandamano hivi karibuni.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI