• Seynation Updates

    Tuesday 30 May 2017

    Ajira za walimu wa masomo ya sanaa zawekwa kiporo.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ameongeza pressure kwa walimu wanaosubiri ajira kwa kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari.
    Related image
    Waziri, Angela Kairuki
    Angela Kairuki amesema kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao kwani kuna walimu wengi wa masomo ya sanaa ambao ni wa ziada kwenye shule za sekondari.
    “Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa ‘redeploy’ kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya.” – alisema Angela Kairuki leo bungeni.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI