• Seynation Updates

    Monday 13 November 2017

    MAMA KANUMBA ASEMA KUWA ANAENDA KUMZIKA UPYA KANUMBA

    MAMA KANUMBA
    Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.


    Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.
    "Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba
    Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.
    Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI