• Seynation Updates

    Thursday, 30 November 2017

    Zimbabwe yajiengua CECAFA

    Chama cha mchezo wa soka nchini Zimbabwe (ZIFA) kimetangaza kujitoa katika kombe la michuano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA ambayo inatarajiwa kuchezwa nchini Kenya kuanzia Desembe 3 hadi 17 mwaka huu.
    Kupitia mtandao wake wa kijamii ZIFA imesema imeamua kujiengua katika michuano hiyo kufuatia kutotengemaa kwa hali ya kiusalama kwa nchi mwenyeji Kenya.
    “Kufuatia mashauriano ya kina na wadau wote, Chama cha mchezo wa soka nchini Zimbabwe (ZIFA) kimeadhimia kujitoa katika kushiriki michuano ya CECAFA Chalenji Cup ya mwaka 2017 kutokana nakutotengemaa kwa hali ya kiusalama kwa nchi mwenyeji Kenya, hivyo basi ZIFA imesimamisha maandalizi yote mara moja  ya kushiriki kama mgeni mualikwa wa mwaka huu.” Imesema ZIFA
    “ZIFA inaahidi kujitolea kushiriki katika mashindano yajayo endapo kama hakutakuwa na hali yoyote ya kiashiria cha ukosefu wa usalama. Kujitoa katika mashindano haya si kitu kizuri kwetu, kwa timu, taifa na hata kwa waandaji wa mashindano wenyewe lakini tulihitaji kufanya uamuzi mgumu kwa maslahi ya wote waliohusika.”
    “ZIFA inafungulia milango wa ushirikiano kwa CECAFA na miili mingine kwasababu kupitia mashindano tunaweza kuimarisha ushindani timu zetu na kuziongezea thamani. Pia tunaomba radhi kwa waandaji wa mashindano, wadhamini, timu, mashabiki pamoja na wadau wote kwa matatizo tutakayokuwa tumeyasababisha kwa kujitoa kwetu ghafla.”
    “ZIFA inaitakia CECAFA michuano bora yam waka huu na mashindano yajayo.”
    Zimbabwe will no longer play in the 2017 CECAFA Challenge Cup to be hosted by Kenya @XolisaniGwesela... http://fb.me/5aWPMuZQD 

    Hapo awali jumla ya mataifa 10 yalitarajiwa kushiriki katika michuano hiyo mikubwa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki sasa baada ya kujitoa Zimbabwe zitakuwa zimesalia jumla ya nchi tisa huku droo ya hatua ya makundi ikionyesha mwenyeji Kenya itacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Rwanda.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI