• Seynation Updates

    Wednesday 20 December 2017

    HAJI MANARA NA UZUSHI WA KIFO.


    Mjadala wa taarifa za kuzushiwa kifo cha Msemaji wa Simba, Haji Manara umeendelea mtandaoni huku wengine wakihoji iko wapi hiyo taarifa aliyozushiwa. 

    Hata hivyo, Manara alitoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo alizozisoma kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kwamba si za kweli kwani ni mzima. 

    Manara alishangazwa na watu kusambaza uvumi huo na alisisitiza kupitia akaunti yake ya Istagram kuwa yeye ni mzima kabisa. 

    Alisema kwamba taarifa hizo ziliwafikia ndugu zake na kuwashtua lakini hazina ukweli.
    Usisahau Ku FOLLOW INSTAGRAM @seynation

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI