• Seynation Updates

    Friday 29 December 2017

    HARMONIZE NA MZUNGU WAKE 'SARAH_TZ' WAGUSWA NA DHIKI ZA WALEMAVU MTWARA WAMETOA MISAADA LUKUKI

    Ikiwa zimebaki siku chache Ili msanii Harmonize kutoka kundi la WCB pamoja na wenzake Kutumbuiza katika uwanja wa Nangwanda-Sijaona nia na madhumuni yao ni kuujaza uwanja huo #TUKAIJAZE_NANGWANDA mnamo tar 31-Desemba mwaka huu, Harmonize pamoja na Mzungu wake Sarah_tz wamebahatika kuwatembelea Ndugu zao wenye matatizo ya kuona au watu wenye ulemavu ma macho na kutoa Msaada wa Vitu Mbalimbali.

    Kwa Mujibu wa Harmonize, alikuwa ni mtu mwenye kuonesha Kuguswa kwa shida na matatizo aliyoyaona kwa Ndugu hao hali iliyo pelekea Kuandika yafuatayo katika ukurasa wake wa Instagram
    "KATIKA KUELEKEA #TUKAIJAZE_NANGWANDA_31_12_2017 NILIBAHATIKA KUKUTANA NA NDUGU ZANGU WENYE MATATIZO YA KUTOKUONA KWA LUGHA NYINGINE NI WATU WASIOONA KUTOKA CHAMA CHA WASIOONA MTWARA (TLB) MTWARA DAAAH INAUMIZA SANA....!!! LAKINI M/MUNGU NDIO MPAJI NA MWENYE MAMLAKA YA KILA JAMBO KAWACHAGUA HAWA NDUGUZETU NA WENGINE WENGI KUWAPA MTIHANI HUU, KWAKWELI WANAHITAJI FARAJA SANA....!!! LICHA YA MISAADA AMBAYO INAWEZA KUTENGUA CHANGAMOTO WALIZONAZO MAANA MACHO DAAAH, SIJUWI UTAYAPA NAFASI GANI KATIKA MWILI WAKO......!!!! KATIKA CHAMA HIKI WAPO WANACHAMA (112) AMBAO WOTE WANAUHITAJI MKUBWA SANA WA FIMBO ZA KUWASAIDIA KUTEMBELEA IDADI YA FIMBO NILIZOKUJA NAZO HAZITOSHELEZI WAMEZIPOKEA LAKINI PIA WAMENIOMBA NILIFIKISHE HILI KWENU WADAU NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KOTE DUNIANI WANAUHITAJI MKUBWA SANA....!!! SIO FIMBO PEKE MAHITAHI NI MENGI SANA....!!!! NIKUOMBE NDUGU YANGU KWACHOCHOTE ALICHOKUBARIKI M/MUNGU WASILIANA KUPITIA NAMBA HIZI 👉 +255658135762 0716797028 🙏 #KONDEBOY"  Aliandika Harmonize.


    Follow Us On Instagram @seynation

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI