• Seynation Updates

    Sunday, 3 December 2017

    Mo Dewji ashinda zabuni ya uwekezaji ndani ya Simba SC.

    Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji amepita katika mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Tsh bilioni 20.
    Dewji ambaye amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau kubwa la Tsh bilioni 20 kupata hisa kwa asilimia 51 ndani ya klabu hiyo amekubaliwa kwa dau hilo kwa kupata hisa 49.
    Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo wa mabadiliko, Jaji Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo.
    “Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” amesema Jaji Mihayo.

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI