• Seynation Updates

    Friday 29 December 2017

    PENZI LA RAYVANNY NA FAYMAH LIPO PALE PALE...MASHABIKI WALIPIGILIA MSUMARI SWALA HILO



    Hivi karibuni kulikuwa na drama za hapa na pale kuwa msanii wa muziki Bongo, Rayvanny ameachana na Baby Mama wake, Fahyma lakini hilo limekuja kuonekana kutokuwa na ukweli wowote mara baada ya msanii huyo kutoa video ya wimbo wake ‘Safari’ ambapo ndani yupo Fahyma.
    Licha ya video hiyo kuthibitisha kuwa penzi bado lipo pale pale, Rayvany pia amepigilia msumari katika hilo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amendika; “Sikukupata kwa Bahati Mbaya Kwanini Nikuache kwa Makusudi NAKUPENDA MAMA,”.
    Katika hatua nyingine mashabiki wa Rayvanny amekuwa na maoni tofauti kuhusiana na drama hiyo na jinsi ilivyomalizika. Haya ni baadhi ya maoni yao kutoka kwenye mtandao wa Instagram;
    ney_faidaIzo Kiki za kuachana ni ujinga mtupu kwan uwez kutoa wimbo mpk Kiki za ivo mxiew
    kilaveelizabethnice kama umelijua hilo maan jua huyo niwa thaman kuliko vyote coz yeye ndio anae jua maumiv yak na fulah yak usimuache mkeo kisa manen ya watu kaka au kwa ugomvi kumbuka wewe ni binadam na yeye wote hamja kamilika vumilianeni saw kaka@rayvanny mpenda San@fahy_rayvanny
    dkng6267Ile ilikua kiki na tulishtukaaa mapemaa
    katotopureUjue siku atakufa mtu na tujue ni kiki
    carrymastorySasa kiki zakuachana za nn Akili kama za darasa la pili
    faizahremix@rayvanny ngoma kali sana kakangu..ila uache kutuchezea akili najua kabisa hamkuwa mumeachana ilikuwa kiki ya hii ngoma na kwakweli tuneisearch sana youtube. Mihela utapata ila naomba na pia mm unisaidie…@faizah kenya.
    Wimbo wa Safari ambayo Rayvanny amemshirikisha Nikki wa Pili amechukua baadhi ya vionjo kutoka kwenye wimbo wa msanii wa dansi Husein Jumbe ‘Mapenzi ya Siri’.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI