• Seynation Updates

    Saturday 30 December 2017

    SHETTA KUMTAYARISHA MWANAE QAYLLAH DHIDI YA VIDUME



    Msanii wa muziki Bongo, Shetta amemueleza mwanae wa kike ‘Qayllah’ jambo la kuwanalo chonjo pindi atapokuwa mkubwa.
    Shetta ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Vumba’ aliyomshirikisha G Nako ametumia ukurasa wake wa Instagram kumueleza Qayllah anatapokuwa mkubwa asikubali kudanganywa na wanaume.
    Mwanangu Najua kuna watu wanakusubiri subiri ukue kue walete mambo yao ya Kukunyapia nyapia Sasa ninachokuhusia mwanangu Baba Yako nina kila kitu asijudanganye Mtu ukaingia laini ukakazika kijinga jinga Kaza mwanangu…. !!
    Msanii huyo anayeonekana kuwa karibu sana na mwanae hivi karibu kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm alikaririwa akisema moja ya vitu alivyokuwa akitamani katika maisha yake ni kujaliwa mtoto akiwa katika umri mdogo.

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI