• Seynation Updates

    Saturday 23 December 2017

    SHUGHULI NZITO YA MESSI KWENYE EL-CLASSICO



    Nyota wa Barcelona Lionel Messi ameendelea kusogeza juu rekodi yake ya kufunga mabao kwenye mechi ya El Clasco inayokutanisha Real Madrid na Barcelona baada ya leo kufunga bao moja na kufikisha jumla ya mabao 25.
    Katika mchezo uliomalizika jioni hii Barcelona imeshinda mabao 3-0 dhidi ya Real Madrid na kufikisha alama 45 ikiwa mbele kwa alama 11 dhidi ya Real Madrid inayoshika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa La Liga ikiwa na alama 31.
    Mabao ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 54, Lionel Messi dakika ya 64 na Alex Vidal dakika ya 90. Bao la Messi limekuwa ni bao la 25 kwenye mechi zake 37 za El Clasco na bao la 15 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
    Timu hizo sasa zimecheza jumla ya mechi 238 ambapo Real Madrid imeshinda mara 95 huku Barcelona ikishinda mara 93 na zikitoka sare mara 49.
    USISAHAU KUFOLLOW INSTAGRAM @seynation

    No comments:

    Post a Comment

    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI