• Seynation Updates

    Saturday 9 December 2017

    Tarehe ya kutoka, bei na orodha ya nyimbo zilizomo kwenye album ya ‘A boy From Tandale’ ya Diamond, zatajwa.

    Hakuna ubishi kwa mwaka huu mashabiki wengi wa muziki walikuwa wanasubiria kwa hamu kuipokea album ya ‘A Boy From Tandale’ ya msanii maarufu zaidi Tanzania, Diamond Platnumz ukweli ni kwamba album hiyo haitatoka mwaka huu tena badala yake itatoka mwakani.
    Album ya ‘A Boy From Tandale’ itatoka tarehe 12 Januari 2018, na itakuwa na nyimbo 18, ambapo zaidi ya wasanii 13 kutoka Tanzania, Nigeria na Marekani watasikika kwenye album hiyo.
    Wasanii hao ni Vanessa Mdee, P-Square, Mr Flavour, Young Killer, Tiwa Savage, Rayvanny, Davido, Jah Prayzer wengine ni Miri Ben-Ari,  Omarion, Rick Ross, Ne-Yo na Morgan Heritage wote kutoka Marekani.
    Kupitia mtandao wa iTunes unaweza ku-order sasa hivi kabla haijatoka album hiyo kwa dola 6.99 sawa na tsh 15,666/=. Kumbuka bei hiyo ni kwa wale watakaonunua album hiyo kabla ya kutoka tarehe 12 Januari, 2017.
    Tazama orodha ya nyimbo hizo hapa chini;


    VIDEO MPYA

    UMBEA MTUPUU

    MAPENZI